Monday, December 16, 2013

KUISHI MAISHA YA USHINDIImekuwa ni matatanio ya kila mwanadamu kuishi maisha ya ushindi lakini hayo matamanio hutofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine hii ni kwa sababu ya mitazamo kutofautiana.Ukisoma katika biblia utaona utaona jinzi Mungu alivyo mkusudia binadamu aishi maisha ya ushindi ndio mana ukiangalia uumbaji wa binadam ni tofauti na uumbaji wa vitu vingine MWANZO 1:6-24 Mungu alipoumba vitu vyote alitamka kiwepo hiki na kikawepo lakini ulipokuja uumbaji wa binadam ulikua katika majadiliano kati ya MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA ROHO MTAKATIFU{TRINITY} Mwanzo 1:26 biblia inasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu wakatawale…………kwa hiyo tunaona dhahiri kwamba Mungu alishirikisha cabinet lake mbinguni katika kumuumba binadam na huyo binadamu aliubwa atawale.Pia uumbaji wa binadam ulikuwa katika process Mwanzo2:7&18&21-22 uumbaji wa binadam ulikuwa katika hatua biblia inatuambia yalichukuliwa mavumbi ya ardhi ambayo yaliumba mtu asie hai, ili mtu awe hai Mungu alimpulizia pumzi yake hatmaye akawa nafsi hai vile vile uumbaji wa HAWA.Kabla sijaendelea na kujikita katika somo ningependa tujiulize ni upi mfano wa mungu kumbuka hatujaubwa kama Mungu lakini tumeubwa kwa mfano wake.Biblia inamuelezea kuwa Mungu ni ROHO Yohana 4:23 Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. Kwahiyo binadamu kuna namna ambayo aweza akaishi kama Roho(kuishi Rohoni).

No comments:

Post a Comment